Wanawake wanadhihirisha kwamba wana ujuzi wa kusakata dimba
Katika soka ya wanawake kufuzu kwa kombe la dunia Uingereza imeichapa Ukrain 4 kwa sufuri ikiwa ni ushindi wa mara ya sita katika kundi lao.
Huku Sweden ikiilima Ireland kazkazini matatu kwa yai katika mechi hizo za jana.
Lakini kama akina dada wanasoka wa Uingereza wamepewa sifa tele kwa ushindi huo mkubwa, manung’uniko yameenea nchini humo kuhusu timu ya wanaume inayotarajiwa kuiwakilisha Uingereza kwenye dimba la kombe la dunia Brazil hapo Juni mwaka huu.
Chama cha soka cha nchini humo kinasema nisharti timu ya Uingereza ijadiliwe kwani jinsi ilivyo sasa huenda wasing’are katika kombe la dunia.
Kumbuka Uingereza ingali inasubiri kushinda kombe la dunia tangu 1966 na mchuano uliopita ilitolewa na Ujerumani raundi ya pili tu huko Afrika kusini miaka minne iliyopita.
Kumbuka Uingereza ingali inasubiri kushinda kombe la dunia tangu 1966 na mchuano uliopita ilitolewa na Ujerumani raundi ya pili tu huko Afrika kusini miaka minne iliyopita.
Kutokana na mahojiano na wadau wa soka zaidi ya 600, imeonekana ipo haja ya kuwapa nafasi zaidi vijana chipukizi walio kati ya miaka 17 and 21 na vilevile kuundwa kwa ligi ya pili ya Premier, yaani Premier League B, ili kukuza vipaji hivyo.
Lakini linalozusha tafrani katika mapendekezo hayo ni lile la kusema , sasa kuwekwe masharti magumu zaidi katika utoaji vibali kwa wachezaji wanaotoka nje ya umoja wa ulaya ndiposa kujenga fursa kwa vijana wa nyumbani.