Sevilla wameshinda kwa mikwaju ya penati na kubeba kombe la Ligi ya Europa dhidi ya Benfica.
Ni miongoni mwa fainali za kusisimua katika michuano hiyo na kila timu ilipata nafasi kadhaa za magoli lakini milango ilibaki ikiwa imefungwa hadi kumalizika dakika 120. Katika kipengele cha penati au bahati na sibu kama ambavyo wadau wengi wa soka hupenda kusema, ndipo mlinda mlango wa Sevilla Beco alipoitunukia kombe timu yake kwa kuokoa penati mbili ikiwemo ya Oscar Cardozo na Rodrigo na kuifanya Sevilla kushinda kwa penati 4-2.
Benfica wanacheza fainali ya nane sasa katika michuano ya Ulaya tangu mwaka1962, na wamepoteza fainali zote. Huenda ikawa ni laana aliyoiacha kocha Bella Guttman baada ya kutimka klabuni hapo na kusema kuwa Benfica hawatashinda kombe lolote katika mashindano ya Ulaya kwa miaka 100.