Wakali kutoka pande tofauti za Africa walifunika ipasavyo ndani ya Club Billcanas, katika show hiyo iliyoandaliwa na MTV Base kama mojawapo ya maandalizi kuelekea katika tukio la tuzo za MTV MAMA zitakazofanyika June 7 huko Durban Afrika Kusini. Mastaa kama Diamond Platnumz kutoka hapahapa kwa Nyerere, Mikasa na Proffesor kutoka kwa Madiba(Afrika Kusini), Sauti Sol kutoka Kenya na wengine wengi walilishambulia jukwaa kama simba katika usiku huo.
Tazama matukio katika picha kwa hisani ya Bongo 5 na Millard Ayo.