Waziri mkuu wa India Narendra Modi |
Chama cha upinzani nchini India BJP kimeshinda uchaguzi mkuu kwa kupata idadi kubwa zaidi ya kura kuliko chama kingine chochote.
Kiongozi wa chama BJP Narendra Modi,amesema kuwa wananchi wajiandae kwa mambo mazuri
Wafuasi wa upinzani wanasherehekeakatika makao makuu ya chama hicho.Matokeo ya awali yalionyesha kuwa chama hicho kimepata kura nyingi kiasi cha kuweza kutawala bila ushirikiano wowote na chama kingine.
Chama tawala cha Congress kimeshindwa baada ya kuwa mamlakani kwa miaka kumi
Kura ambazo zimehesabiwa kufikia sasa zinaonyesha kuwa muungano wa vyama unaoongozwa na chama BJP, chini ya Bwana Narendra Modi, utashinda kwa wingi wa kura.
Tayari shangwe, vifijo na nderemo vimeshuhudiwa na kusikika katika makao makuu ya BJP huku wanachama wakicheza densi barabarani na fataki kulipuliwa.
Tume ya Uchaguzi ya India imesema kuwa matokeo ya awali yanathibitisha kuwa BJP kimeshinda viti 272, vinavyokiwezesha kutawala bila kushirikiana na chama kingine.
Zaidi ya watu milioni 500 walipiga kura ambayo ni asilimia 66 ya wote waliochaguliwa.
BBC