Wengi wanapnda kumuita CR7, Christiano Ronaldo ambaye ndiye mchezaji bora Ulimwenguni kote, ameendelea kuvunja rekodi katika soka la Hispania kwa kutwaa tunzo ya PACHICHI.
Tunzo hii hutolewa kwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi katika msimu wa Laliga.Ronaldo amefunga mabao 30 katika mechi 31 alizoichezea timu yake ya Real Madrid atka msimu uliomalizika wa Laliga.
Amempiku mpinzani wake mkubwa Lionel Messi na Diego Costa ambao walimpa ushindani katika mbio za kuwania tunzo hiyo. Ronaldo pia anaongoza kwa magoli katka michuano ya UEFA akiwa na magoli 16 huku akiwa amebakiza mchezo wa fainali.
Pia Ronaldo ameingia katika kinyang’anyiro cha kuwania tunzo ya mfungaji bora wa ligi zote za Ulaya akichuana vikali na Luis Suarez wa Liverpool.