Ronaldo na mpenzi wake Irina Shayk wamepata nafasi ya kuwa katika photo cover ya magazine kubwa huko nchini Hispania ambapo Ronaldo ametokeza akiwa hajatinga vazi la aina yoyote na sehemu kuu ya siri ikiwa imezuiliwa na mpenzi wake Irina Shayk ambaye yuko mbele yake katika picha hiyo.
Wawili hao wameendana vyema ingawa hawatabiriwi kuwashinda Kanye West na Kim Kardashian ambao walivuma sana katika toleo lililopita la jarida hilo.
Mwanamitindo Shayk alivuma katika vyombo vya habari siku za karibuni kwa kutumia picha ya utupu kupinga vitendo walivyofanyiwa wasichana wa Nigeria na Boko Haram,maarufu kama #BringBackOurGirls.
Ronaldo na Shayk walianza mahusiano yao ya kimapenzi tangu mwaka 2010 na bado wanajivunia mahusiano yao mpaka sasa.