Mholanzi Lous Van Gaal ambaye anainoa timu yake ya taifa ya Uholanzi ametangazwa rasmi mchana wa leo kuwa kocha mkuu wa Manchester United akiziba pengo la David Moyes ambaye alitimuliwa klabuni hapo mapema Aprili kufuatia mwenendo mbaya wa kikosi cha mashetani wekundu. Mdachi huyo atasaidiana na Ryan Giss ambaye ni mchezji mkongwe klabuni hapo na ambaye aliteuliwa kuwa kocha mkuu kwa muda.
Van Gaal atakuwa Brazil na kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi, lakini baada ya michuano hiyo ataanza rasmi kibarua katika klabu ya Man U. Makubaliano ya Van Gaal na United yalifikiwa tangu Aprili 26 lakini kutangazwa kwake rasmi kulicheleweshwa makusudi, ili kumpa nafasi Van Gaal kutafakari kwa kina juu ya muafaka wake na timu ya taifa ya Uholanzi.
Van Gaal amesaini mkataba wa miaka mitatu kuinoa United na ameripotiwa na mtandao wa Goal.com kuwa “mwenyewe nilivutiwa kuinoa Man U baada ya Moyes kuachishwa kazi”
Mkuu wa United, Ed Woodward amesema “tumeipata huduma ya moja ya makocha bora Duniani, ana mafanikio makubwa katika kazi yake, na Old Trafford ni jukwaa linalomfaa na linaompa nafasi ya kuandika kurasa mpya za historia ya Man U.
“Kila mmoja anafurahishwa na hatua hii nzuri katika historia ya United. Historia yake nzuri ya kushinda vikombe mbalimbali vya ligi na michuano ya Ulaya,inamfanya awe chaguo letu sahihi”
Van Gaal amesma ” najihisi fahari kufanya kazi na Manchester United klabu kubwa Duniani nikiwa kama kocha mkuu”.