MAMAA Majanga, Snura Mushi amekiri kutoka katika uvungu wa moyo wake kuwa amedhibitiwa vilivyo na penzi la jamaa anayetoka naye kwa sasa aitwaye DJ Hunter hivyo hawezi kuachika.
Akipiga stori na mwandishi wetu, Snura alifunguka kwamba tofauti na wanaume wote aliowahi kuwa nao, DJ Hunter wanapendana kwa dhati na anaamini ndiyo chaguo sahihi kwake. “Sijawahi kuwa na mpenzi nikamtambulisha kwenye media bila kuwa nimempenda kwa dhati, tunapendana sana na Hunter, hatuwezi kuachana kwa mipango ya binadamu,” alisema Snura.
chanzo; GPL