Ukiongelea watu maarufu hapa town, ni wazi kwamba Wema ndiye maarufu zaidi kuliko celebrity yeyote yule wa kike hapa bongo, cause kila rika linamjua Wema Sepetu, na haswa vijana wengi wa kike hutokea kumpenda sana Diva huyu, ila tukienda kwa level zakimataifa hapo kidogo ndio utata unapokuja haswa ukilinganisha na presenter maarufu hapa town na mwanamuziki mkali wa Come Over yaani Vanessa Mdee. Haina budi tukubaliane na ukweli kwamba, yuko famous zaidi ki-international zaidi kuliko mtu mwingine anavyodhani kwa mtazamo wa haraka haraka hapa Bongo.
Vanessa akiwa na Jay-z(Mr.Carter)
Vanessa ni moja ya msanii wa kike ambaye mbali tu na umaarufu wake huo kimataifa bali, ana ule muonekano wa ki-star, kitu ambacho ni nadra sana kukipata kwa wasanii wengi hapa Bongo, ila tukirudi kwa Wema Sepetu ambaye ndiye ana-run industry ya watu maarufu hapa Bongo , upande wa wanawake, ukilinganisha na Vanessa Mdee bado jibu utapata kuwa Vanessa ndie anayekimbiza kwa upande wa muonekano wakistar na umaarufu wa kimataifa zaidi ukilinganisha na wa hapa Bongo.Pia kingine cha tofauti kwa Vanessa Mdee kimataifa ni kitando cha Raisi wa Marekani , Barack Obama kum-followVanessa Mdee kupitia mtandao wa twitter , kitu ambacho kinaonesha kwa kiasi gani Vanessa ni mtu mkubwa kimataifa ukilinganisha Bongo. Hata hivyo bado anaendelea kuja juu kwa hapa Bongo, kwa kuendelea kula dili mbali mbali zitakazo Boost umaarufu wake hapa kwa hapa Bongo, ikiwemo umaarufu anaozidi kupata kupitia muziki wake na dili nyingi za matangazo anazoendelea kupata.