Mtandao wa habari wa MailOnline umevujishiwa video inayoonesha mastaa hao wawili wa kundi maarufu la muziki wa Pop kutoka nchini Uingereza wakivuta bangi wakati wakiwa wanakata mitaaa nchini Peru.
Video hiyo inawaonesha wakali hao wakigongeana ganja wakiwa katika gari.
Baadhi ya mashabiki wamekerwa na kitendo hicho na kusababisha kulichukia kundi hilo wakali wa “Story of My Life” na baadhi wamepost picha wakionesha ishara ya kuchoma tiketi za show za One Direction.
Mwakilishi wa bendi hiyo ya muziki yenye jumla ya waimbaji watano, ameuambia mtandao wa TMZ kuwa, video hiyo iliyoonekana kwenye mtandao wa MailOnline imeibwa na kuvujishwa na mwanasheria wao analifanyia uchunguzi suala hilo.