Alikiba, wamekuwa wakijiuliza sababu zilizomfanya mwimbaji huyo kukaa
kando ya muziki kwa muda mrefu.
Novemba 2012 hajawahi kuachia tena wimbo mwingine, licha ya kutoa kazi
kadhaa alizokuwa akishirikishwa na mdogo wake msanii Abdu Kiba ukiwamo
“Kidela”.
wa kwanza “Sinderela” mwaka 2007, nyumbani kwake Kunduchi Beach na
ambapo aliainisha mambo makubwa matatu yaliyomfanya asimame kwa muda
kuachia kazi za muziki.
“Kuna mambo
matatu ya msingi niliyokuwa nayafanya kwa kipindi hiki cha miaka mitatu.
Awali ya yote niliamua kusimama ili kumlea mwanangu, malezi ya mtoto
yalinifanya niegemee huko hadi umri wake usogee ndipo nirudi kwenye
muziki,” anasema pasipo kufafanua vizuri iwapo ni wa kike au wa kiume.
“Jambo la pili
ambalo najivunia kulifanikisha kwa kipindi hiki, ni kuweza kumsimamisha
sehemu nzuri mdogo wangu Abdu Kiba katika ramani ya muziki. Hili
lilikuwa suala kubwa na nyeti kwangu kuhakikisha anatimiza ndoto zake
nilijitahidi kumpa nyenzo ili na yeye ajulikane kwani nilimuona ana
kipaji kikubwa,” anasema.
atakavyowaacha wasanii wengine Tanzania, na wao wajulikane ndani na nje
ya nchi.
“Tatu niliona
nitulize kichwa kidogo kwa kufanya biashara na pia kuwaacha wasanii
wengine na wao kipaji chao kionekane na kuwapa nafasi ya kufanya vizuri
ndani na nje ya nchi, nashukuru hilo limefanikiwa tena kwa kiasi
kikubwa, kwa kuwa kwa kipindi hicho wameibuka wengi ambao wameweza
kufanya vizuri na kwa wale ambao walikuwepo kitambo wamepanuka zaidi
kifikra,” anasema Alikiba.
na pia ameona kumekuwa na mapungufu katika tasnia ya muziki wa kizazi
kipya na maendeleo pia.
ya wasanii wamefanikiwa kufanya muziki mzuri na kuutangaza kimataifa na
wengine wametengeneza kazi nzuri, lakini kinachonitisha ladha ya muziki
wetu asili hasa ya bongofleva, imepotea tumeanza kutengeneza muziki
wenye utofauti mkubwa sana na kipindi cha nyuma, kwa kuiga ala ya muziki
wa Nigeria na mataifa mengine,” anasema Alikiba.
Albamu mbili, singo mpya wiki ijayo
ameweka wazi ujio wake wiki ijayo akiwa chini ya kampuni kubwa barani
Afrika ambayo hajataka kuiweka wazi, anasema alikuwa ‘chimbo’ kwa
takribani miaka miwili akiandaa kazi mpya ambapo amefanikiwa kukamilisha
albamu mbili na punde kuachia singo mpya.