Mtoto wa miaka 14 wa mwanamuziki mkongwe wa R&B wa nchini
Marekani R Kelly ametangaza kubadilisha jinsia yake kupitia mitandao ya
kijamii.
Mtoto huyo aitwaye Jaya alizaliwa mwanamke lakini akachukua uamuzi
mgumu na kuwaambia mashabiki zake kuwa sasa hivi yeye ni mwanaume
akiitwa Jay kwakuwa amebadilisha jinsia yake.
Lakini wakati mama yake Andrea Kelly akimuunga mkono mtoto wake
kutokana na hatua hiyo, baba yake R Kelly bado hajazungumza chochote.
Jaya ambaye sasa anaitwa Jay amesema mama yake alifurahishwa sana kwa
kitendo chake hicho na kusema anampenda mtoto wake vyovyote vile alivyo
ambapo anamshukuru mama yake kwa kukubali yeye kubadili jinsia yake na
kuwa mwanaume.
Ameongeza kuwa anaamini yeye sasa ni mwanaume na anataka upasuaji zaidi na tiba ya kumsaidia kuwa vile alivyotakiwa.
Jay amesema akiwa na umri wa miaka sita alijigundua kuwa anavutiwa sana na wasichana lakini hataki mahusiano kwanza.