Wakati mashabiki wa Uruguayi wakifurahia kufuzu kwa timu yao kwenda hatua ya pili ya michuano ya kombe la Dunia inayoendelea huko nchini Brazili baada ya jana kuipiga Italia kipigo cha bao moja bila. Mshambuliaji wao tegemezi ambaye pia ni mchezji na mfungaji bora wa msimu uliomalizika wa ligi kuu ya Uingereza ameingia matatizoni baada ya mlinzi wa timu ya Italia Giorgio Chiellini kudai kung’atwa na mchezaji huyo begani.
Vyombo vingi vya habari vimepambwa na habari hiyo, na tayari shirikisho la soka la Dunia, FIFA limeweka wazi kuwa uchunguzi unafanyika na endapo itabainika kuwa kweli alimng’ata, atachukuliwa hatua ya kuvunja vipengele viwili vya kanuni za mashindano, kwanza cha utovu wa nidhamu na pili kukiuka fair play.
Kwa upande wa Italia wao wamemlalamika muamuzi wa mchezo kwa kushindwa kutoa maamuzi sahihi baada ya kumtoa kiungo mshambuliaji wa Italia Claudio Marchisio kwa kumuonesha kadi nyekundu na kutochukua hatua yoyote kwa Luiz Suarez ambaye anadaiwa na pia video zinaonesha jinsi alivyomng’ata suarezi.
Chiellini kwa upande wake anaamini FIFA watafanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua zinazopaswa. Wakati Suarezi wakati alipoulizwa na mwamuzi juu ya madai ya Chiellini alisema, “hizo ni hali ambazo hutoke uwanjani, kwani wote tulikuwa kwenye boksi na akanisukuma kwa bega”
FIFA katika kanuni zake wanaruhusu mkanda wa video kutumika katika kumwadhibu mchezaji na kama itabainika kuwa kweli basi hii itakuwa ni mara ya tatu kwa Suarez kuwang’ata wachezaji wenzake. Aliwahi kumng’ata Branislav Ivanovic wa Chelsea na Otman Bakkal wa PSV Eindhoven.