Katika jambo lililotokea kama suprize flani hivi, kwa mara ya kwanza katika historia ya muziki wa bongo fleva, nyimbo ya Diamond Platnumz “Mynumber1″ ilienda hewani jana kupitia television hiyo ya kimataifa ya BET, DiamondPlatnumz anaweka historia mpya tena kuonekana katika kituo hicho cha television, ikiwa haijawahi kutokea kwa mwanamuziki yeyote kutoka bongo kufikisha nyimbo yake level hizo na kufanikiwa kupigwa katika kituo hicho cha television kinachoangaliwa na maelfu ya watazamaji duniani kote. Diamond Platnumz amefungua pazia kwa dunia kuanza kuangalia vipaji vingine kutoka tzee, ikiwa huu ndio mwanzo tu wa mafanikio, akiwa ndiye msanii anayeongoza na kufungua kila njia ya historia mpya ya muziki wa bongo.