Na Khadija Mngwai
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij, amemuondoa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa katika kikosi chake kitakachoivaa Msumbiji.
Sababu kubwa iliyotajwa ni Ngassa kushindwa kuripoti katika kikosi
hicho wakati alipoitwa kucheza dhidi ya Botswana kabla ya kuivaa
Msumbiji katika kuwania kushiriki Kombe la Mataifa Afrika (AFCON).
Chanzo
cha habari kutoka ndani ya benchi la ufundi la Stars, kimesema kuwa
Ngassa alikaidi wito wa kocha huyo, ndiyo maana akamkasirisha.
“Kocha hatamtumia Ngassa katika mechi ijayo dhidi ya Msumbiji,”
kilisema chanzo hicho. Alipoulizwa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Selestine Mwesigwa alisema hawana taarifa yoyote juu ya
kutokuwepo kambini kwa mchezaji huyo.
“TFF haihusiki kwa namna yoyote juu ya kuondoka kwa Ngassa, kwani
mamlaka yote yapo kwa klabu yake ambayo ndiyo inammiliki,” alisema
Mwesigwa.
Maximo kuwaongoza mashabiki Yanga kuishangilia