Mwimbaji tishio zaidi katika bendi ya muziki wa miondoko ya pop na rock ijulikanayo kama Maroon 5, Adam Levine siku ya leo anatarajia kuungana na wanandoa kote ulimwenguni, kwani leo ndio yeye na mwanadada mrembo Behati Prinsloo watahalaliswa kuwa mwili mmoja. Mrembo Behati Prinsloo ni mwanamitindo wa Victorias Secret.
Harusi hiyo itafanyika leo katika ukumbi wa Cabo San Lucas, Mexico na mpiga kinanda wa bendi hiyo, Jesse Carmchael ndiye atakuwa Best Man wa Adam. Kama ni mfuatiliajiwa Band hii utaona nyimbo nyingi Adam amekuwa akitawala sehemu kubwa, wimbo kama “Payphone” ni kielelezo tosha.