Beyonce Knowles mwimbaji ambaye kwa mwaka huu amekuwa na mafanikio zaidi katika muziki amepata shavu la kutuzwa tuzo ya Video ya Mwanamuziki anayeongoza kwa kuwa na Video kali zaidi, “Video Vanguard Award” ambayo inashikiliwa na mfalme wa Pop Duniani, hayati Michael Jackson.
Beyonce atatunukiwa tuzo hiyo kutoka kwa MTV katika sherehe za tuzo za Video za Muziki (VMA), zinazoandaliwa na MTV Base.
Katika tuzo hizo Beyonce anaongoza kwa kuwa katika vipengele nane (8) tofauti na pia ni mmoja kati ya wanamuziki watakaotumbuiza katia sherehe hizo zitakazofanyika tarehe 24 Agosti, 2014. Beyonce atatumbuiza katika tuzo hizo kwa mara ya kwanza tangu atangaze kuwa mjanzito mwaka 2011, na wasanii wengine akiwemo Usher Rymond, Ariana Grande na Zedd watapagawisha katika sherehe hizo.
Tunzo hiyo ya “Video Vanguard Award” pia imewahi kutunukiwa wakali kama, Justin Timberlake, Britney Spears, Janet Jackson, Madonna, na mkali wa Pop, Michael Jackson.