Mkali wa Bongo fleva ambae wimbo wake wa niende zangu bado haujachuja ameamua kuwapa mashabiki wake ladha nyingini kwa kuachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la “Nakumiss miss”. Timbulo amepost kwenye ukurasa wake wa facebook na ameweka namba yake kwa yeyote anayehitaji kutumiwa wimbo huu kwa njia ya whatsapp. Ni wimbo wa kuchezeka ambao ameufanya kwa Mazuu Records na ni mkali na kwa vile masikio hayadanganywi, usikilize mwenyewe hapa: