Akiongea kwenye mahojiano na Bongo5, Vanessa amesema ushindi wa
Diamond kwenye tuzo za Channel O ulikuwa mkubwa kiasi cha kuwaogopesha
wasanii hao na kwamba hawakutarajia ushindi kama huo kutoka kwa msanii
wa Tanzania.
“Nilipata bahati ya kukaa siti za mbele kwenye tuzo za Channel O,na
nyuma yangu walikuwa wamekaa wasanii wengi wa Kinaijeria. Kila alipokuwa
anashinda Chibu tunasimama tunamshangilia, nilikuwa nimekaa na Victoria
Kimani na msanii mmoja wa Kenya anaitwa Yvonne Darq, tunasimama
tunamshangilia, ni ndugu yetu, ni rafiki yetu na anatutengenezea vitu
fulani hivi,” amesema Vanessa.
“Kwenye kusimama kwetu na kushangalia wale watu walikuwa wanaumia
fulani hivi. It was so strange, nawatizama nasema ‘jamani najua mmezoea
kushinda na ninajua mnaogopa vile ambavyo hamvielewi but just celebrate
kwani kuna tatizo gani’. I think they are shocked, at the same time
wanajaribu kuelewa what we are doing right and what they are doing
well.”
“But kusema ukweli wamefanya vizuri sana wenzetu katika muziki katika
this past few years but if you look back, muziki wa Bongo Flava ulikuwa
ni mkubwa zaidi na ulikuwa ushadevelop vitu fulani kabla ya Wanaijeria
hawaja popular on the African scene so I think it’s time to reclaim the
throne.”