Baada ya sikukuu ya Christmas December 25, tumeona mitandaoni watu
wakifurahia siku ya jana kwa kupokea zawadi mbalimbali toka kwa wapenzi,
ndugu, jamaa na marafiki zao.
wakifurahia siku ya jana kwa kupokea zawadi mbalimbali toka kwa wapenzi,
ndugu, jamaa na marafiki zao.
Sio Bongo tu kulikuwa na mastory ya kupeana zawadi, kutoka Marekani rapper Ludacris ameona isiwe kesi, nae katoa zawadi kwa mpenziwe.
Boxing day ya 2014 itakuwa historia kwenye maisha ya Ludacris na mpenzi wake Eudoxie Agnan kwa kuwa wapenzi hao walifanya engagement, Eudoxie alivishwa pete ya uchumba baada ya uhusiano wao kuwa hai kwa miaka mingi kama wapenzi wa kawaida.
Ludacris aliwaalika marafiki kadhaa akiwemo Star LeToya Luckett kutoka
kundi la Destiny’s Child, na kusafiri nao kutoka Atlanta kuelekea Costa
Rica kwa ndege ya kukodi, ndege ilipoanza kupaa Ludacris alimwambia
mpenzi wake aangalie dirishani, kulikuwa na maneno yaliyoandikwa ‘Will you marry me?’, Eudoxie hakuwa na neno nje ya kujibu kwa furaha ‘ndiyo‘.

Ludacris alishare picha za tukio hilo katika ukurasa wake wa Instagram na kuandika “She didn’t say yes. She said HELL YES! #milehighproposal”