Mwaka wa 2014 ulikuwa mwaka mzuri kwa nyota wa Muziki wa Pop Taylor
Swift baada ya mwanamuziki huyo kumaliza akiwa ameongoza kwenye orodha
ya wasanii waliouza albamu nyingi nchini Marekani .
Kwa mujibu wa kampuni ya Nielsen Music , Albamu ya 1989 iliyotolewa
na Swift mwneye umri wa miaka 25 iliuza jumla ya nakala milioni 3.6
idadi ambayo ilikuwa kubwa kwa kopi za albamu zote kwa mwaka 2014.
Albamu ya the Frozen ambayo nyimbo zake zilitumika kwenye movie ya
The Crown ilifuatia kwa mauzo ikiwa imeuza nakala milioni 3.53.
Cha ajabu ni kwamba albamu hii ya The Crown iliongoza kwa mauzio kwa
kipindi cha miezi 12 kabla ya kupitwa kwenye mauzo kati wiki za mwisho
za mwezi desemba ambapo ilipitwa na albamu ya Taylor Swift baada ya
albamu hiyo ya 1989 kuuza kopi 326,000 katika kipindi cha wiki moja.
Alabmu hizi mbili ndio albamu pekee zilizofanikiwa kuuza kopi milioni 3 kwa kipindi cha mwaka 2014 .
Albamu ya tatu ilikuwa albamu ya Sam Smith iliyoitwa The Lonely Hour
ambayo iliuza kopi milioni 1.21 ikifuatiwa na albamu za Beyonce , Lorde
na One Direction pamoja na albamu ya mwanamuziki mkongwe Barbara
Streisand
Disney Music Group ambao walisimamia albamu ambazo zimetumika kama
soundtrack kwenye movie za Frozen na Guardians of The Galaxy
wamefanikiwa kuingiza albamu mbili kwenye albamu tano bora kwa mara ya
kwanza kwenye historia ya takwimu za Nielsen Music .
Hii ni mara ya pili kwa Taylor Swift kumaliza mwaka akiwa na albamu
bora kimauzo kwa Marekani baada ya albamu yake ya mwaka 2009 ya Fearless
kumaliza ikiwa juu baada ya kuuza kopi milioni 3.22
Chati Rasmi ya Albamu Za Marekani kwa Mwaka 2014
1.Taylor Swift – ‘1989’
2.Disney Music Group – ‘Frozen’ soundtrack
3.Sam Smith – ‘In the Lonely Hour’
4.Pentatonix – ‘That’s Christmas To Me’
5.Disney’s Hollywood Records – ‘Guardians of the Galaxy’ soundtrack
6.Beyoncé – ‘Beyoncé’
7.Barbra Streisand – ‘Partners’
8.Lorde – ‘Pure Heroine’
9.One Direction – ‘Four’
10.Eric Church – ‘The Outsiders’