WAKATI baadhi ya wasanii wa hapa jijini, Dar wakifa
huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni tofauti kwa nyota wa filamu na
muziki, Baby Madaha baada ya kufunguka kuwa akitokea amekufa hataki
kuzikwa Dar na badala yake azikiwe jijini, Mwanza.
huzikwa hapahapa, jambo hilo limekuwa ni tofauti kwa nyota wa filamu na
muziki, Baby Madaha baada ya kufunguka kuwa akitokea amekufa hataki
kuzikwa Dar na badala yake azikiwe jijini, Mwanza.
Akizungumza na Uwazi, Madaha alisema kuwa hajui kifo chake kitatokea
lini na anachotaka ni kutimiza yale aliyopewa kama wosia na marehemu
baba yake ambaye alizikwa jijini Mwanza. “Nasema ukweli sitaki kuzikwa
Dar hasa kwenye makaburi ya Kinondoni, nahitaji kupelekwa nyumbani,
wasanii wenzangu wanatakiwa kujua hilo pamoja na ndugu zangu pia,
naamini kwamba marehemu baba yangu huko aliko ataona ni vizuri mimi
kulala karibu yake kama alivyoniachia wosia huo,” alisema Madah
CHANZO; GPL