Kuna habari nyingi zimekuwa zikimuandama Justine Bieber mwezi huu wa Januari. Habari zote zimetokana na dili la kutengeneza matangazo kutoka kwa kampuni ya mavazi ya Calvin Klein.
Mtandao ujulikanao kama BreathHeavy.com umeingia kwenye libeneke la kumchafua mwimbaji huyo wa Confident baada ya kupost picha zake ambazo hakuziruhusu. Picha hizo zinasadikika kuwa halisi tofauti na zile zinazoonekana kwenye tangazo, ingawa Bieber amekanusha na kusema picha hizo ni feki.
Timu ya wanasheria wa msanii huyo ilitishia kuufungulia mtandao huo kesi ya kumchafua ingawa ilichukua muda mchache baadaye kwa mtandao huo kuomba msamaha.
BreathHeavy.com imeandika hivi “ni kweli Bieber amezikataa picha, naliheshimu hilo na ninamwamini”
Hizi ni baadhi ya picha nyingine za JB akitangaza bidhaa za Calvin Klein.