Mwanadada mkali wa Hip hop anayekinukisha kutoka pande za U.S.A amejikuta katika wimbi la kuandamwa kuhusu staili yake ya muziki na utamaduni wa Hip hop. Ishu hii imeibuliwa na mwanadada Azealia Banks ambaye anaonekana kumpinga wazi wazi Iggy kwa kupost msimamo wake kwenye muziki wa Hip hop na jinsi anavyothamini asili ya muziki huo.
Mwanzoni rapa Lupe Fiasco alisimama kumtetea Iggy na sasa mkali mwingine wa muziki huo, Kendrick Lamar ameibuka na kumtetea mkali huyo wa Black Widow.
Akihojiwa na Billboard Kendrick alisema haya “Iggy anafanya mambo yake, mwacheni”. Watu hujaribu mambo tofauti na hupitia magumu hadi kufika walipo. Fanya mambo yako, endelea kubamba, kwa sababu Mungu anapenda uwe mahali ulipo”.
Kuzungumza kwa Kendrick Lamar kunaweza kusababisha mjadala huu kukua zaidi hasa ukizingatia Iggy ametangazwa kuwania tuzo ya Grammy katika kipengele cha Albamu bora ya Rap.