Staa wa Bongo Movies, Wema Sepetu amekataa kuwa amerudiana na
mpenzi wake wa zamani Chaz Baba japo amedai kuwa muimbaji huyo wa muziki
wa band ndiye mwanaume wa pekee ambaye hakuwa na masuala ya kiswazi baada ya kuachana.
Wema ameiambia U Heard ya Clouds FM Jumatano hii kuwa Chaz Baba kwa sasa ni mshkaji wake na hata alipooa alimchangia pesa.
“Chaz Baba alikuwa ni msikaji wangu naweza kusema ndio boyfriend
pekee asiye na mambo ya Kiswahili,” amesema. “Tulizinguana tukafika
pointi tukasaidiana, ameoa nikamtolea mchango, nimeenda kwenye harusi
yake sioni tatizo.”
“Mimi na Chaz Baba tulikuwa tunapendana na baada ya kufikia point ya
kuachana tukaachana, tukawa hatuongei for sometime mwisho wa siku baada
ya kila mmoja kukaa kwake tukawa tunazungumza. Sio kama watu wengine
tukigombanaga tunatafuta mabifu, hatusemeshani,” alisema mrembo huyo
na kusisitiza kwasasa hana bwana …‘sina bwana’ alisema.