Abdu Bonge alifariki jana Nyumbani majira ya Jioni alipokuwa akiamulia ugomvi wa watu wake wa karibu ndipo alianguka vibaya kwenye sakafu na kupoteza maisha, Mwili bado uko hospitali kwa uchunguzi zaidi na taratibu zikikamilika kesho mwili utasafirishwa kuelekea Morogoro Mbuyuni Kilometa takribani 100 kutokea Morogoro Mjini ambako ni Nyumbani kwa Marehemu. kwa sasa msiba upo Magomeni Njiapanda ya Kagera maskani ya Tiptop Connection
MB Doggy Msanii kutoka TipTop Connection akizungumza jambo na Rafiki waliotembelea Msibani hapo.
Mkubwa Fella akipitisha Daftari la michango kwa Ndugu na Jamaa waliofika Msibani.
Mdogo wa Marehemu Mjomba Iddi mwenye Fulana Nyekundu akizungumza jambo na Rafiki Msibani hapo.
Tunda man akilia kwa Uchungu kabisa akiwa na Babu Tale Msibani Magomeni Njia panda ya Kagera Maskani ya Tiptop Connection.
KWA HISANI YA HARAKATI ZA BONGO