Mwanadada Kat Deluna ambaye amewahi kutamba sana kunako anga za muziki amerejea baada ya ukimya uliokithiri kwa kuachia wimbo mpya akiwa amemshirikisha Trey Songz.
Mwanadada huyo ambaye ni mzaliwa wa Dominic alisikika katika muziki miaka mitano iliyopita kwa nyimbo kali kama ‘I am Dreaming’ na sasa ameamua kusample wimbo wenye mahadhi ya rege wa mkongwe Sister Nancy ‘Bam Bam’ na kutengeneza bonge la kazi linalokwenda kwa jina la ‘Bum Bum’.
“Ninafuraha sana kwa Dunia kusikiliza wimbo wangu mzuri wa ‘Bum Bum’ nikiwa nimeshirikiana na mkali Trey Songz”, “Amesema Kat Deluna wakati akihojiwa na mtandao wa Rap Up. Wimbo huu ni ushahidi kuwa muziki huishi katika vizazi tofauti na kwa hili napenda nimpe pongezi za pekee kabisa Sister Nancy kwa kutunga wimbo mzuri kama huu ambao utaendelea kudumu kwa vizazi vingi vijavyo”. “Naamini ‘Bum Bum’ utakuwa wimbo wako wa msimu”.