Na Imelda Mtema
Beautiful Onyinye wa Bongo, Wema Sepetu amefunguka kuwa, anajua siku zote yeye hana bahati ya kuwa na marafiki kwa kuwa hata akiwa nao mwishowe kunatokea mgogoro na kuachana huku kila mmoja akimuona mbaya
Akizungumza na gazeti hili juzi, Wema alisema anaumia sana kwa kuwa mara nyingi anawapenda sana rafiki zake kwa moyo mmoja lakini mwisho wa urafiki wao huwa ni mbaya sana tena huvunjika kwa kugombana.
“Mimi nimeshajiona siku nyingi sina bahati kabisa, hata nikiwa na marafiki ambao nawapenda kutoka moyoni, mara nyingi wananigeuka na mama yangu amekuwa akinisihi mara nyingi sana, sasa naona bora nifuate ushauri ambao mama yangu ananishauri wa kuangalia watu wa kuanzisha urafiki nao,” alisema Wema