Muigizaji Steven Jacob, ‘JB’ amesema watampigania muigizaji mwenzao, Steven Mangele, ‘Steve Nyerere’ kutwaa ubunge wa jimbo la Kinondoni.
Steve Nyerere ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo hilo, linaloshikiliwa na Idd Azan kwa sasa.
JB alisema wasanii wameungana ili kuhakikisha mwenzao anatinga bungeni.
Wiki iliyopita Steve Nyerere, alifanya mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na nyota wa Bongo Movie.