HABARI za vipigo miongoni mwa wanandoa nyota na kuvunjika kwa ndoa zao zimekuwa zikiongezeka kila kukicha nchini Nigeria, jambo ambalo limemfanya mwanamuziki Peter Okoye wa kundi la P-Square kulivalia njuga akitaka likome.
Katika kuonyesha anavyochukia hali hiyo, Okoye ametengeneza T-Shirt inayolaani ‘Vipigo Majumbani kwa Wanandoa’.
Katika tukio moja la namna hiyo hivi majuzi ni pale mtangazaji wa Cool FM OAP Freeze aliposema kwamba mkewe amekuwa akimpiga kila mara na kumsababishia makovu.
Katika tukio moja la namna hiyo hivi majuzi ni pale mtangazaji wa Cool FM OAP Freeze aliposema kwamba mkewe amekuwa akimpiga kila mara na kumsababishia makovu.
Vilevile ndoa ya mwigizaji maarufu wa Nigeria, Emeka Ike iko shakani baada ya mkewe kudai talaka kutokana na manyanyaso anayofanyiwa na mumewe huyo.
Pamoja na picha ambayo amevaa T-Shirt na kuiweka kwenye mtandao wa Instagram, Okoye aliongeza maneno: “Nyumba ambayo mwanamke hayuko salama si nyumba ya kuishi.
Wanaume pia nao hujikuta wakikutana na vipigo kutoka kwa wake zao. Si wanawake tu ambao huathirika na vipigo, bali wanaume pia huathirika na matusi na maudhi mbalimbali – lakini huogopa kuomba msaada.”