Vijana kutoka Tanzania wakiawa katika picha ya pamoja na msanii kutoka Marekani Ne-Yo wakati wa onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
Msanii wa bongo fleva Ali Kiba akiwa na msichana wa kitanzania Patricia Kajange wakati wa onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
Msanii wa bongo fleva Ali Kiba akiwa na msichana wa kitanzania Barbara Mawalla wakati wa onyesho la Coke Studio Afrika msimu wa tatu lililofanyika hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya.
*********
Kampuni ya Coca-Cola kwa mara nyingine tena kupitia kampeni yake ya ‘Sababu Bilioni za Kuamini’, wiki hii iliwapeleka vijana watano wa Kitanzania kwenda nchini Kenya kushudia onyesho la Coke Studio Africa msimu wa tatu ambapo, msanii maarufu duniani wa miondoko ya R&B kutoka Marekani, Ne-Yo, alitumbuiza pamoja na wasanii wengine kutoka barai Afrika.
Wasanii kutoka Afrika ambao waliungana na Ne-Yo katika onyesho hilo wametoka katika mataifa matano. Wasanii hao ni Ali Kiba(Tanzania), Wangechi (Kenya), Maurice Kirya (Uganda), Ice Prince (Nigeria) na Dama Do Bling (Msumbiji).
Onesho hilo ambao lilikuwa na msisimko wa aina yake kutokana na uwepo wa Ne-Yo, si tu lilivuta hisia za mashabiki waliokuwa wakishuhudia studioni hapo bali pia mamilioni ya wapenda mziki barani Afrika hasa kutokana na ujio wa nguli huyo wa R&B ambaye mziki wake una mvuto wa aina yake.
Vijana hao ambao ni Patricia Kajange, Anderson Dickson, Annalisa Kiango, Barbara Mawalla pamoja na Hilda Steven walionekana kuvutiwa na onyesho hilo na kumimina shukarni zao kwa Coca-Cola kwa kuwapa fursa hiyo ambayo ama hakika wamethibitisha kujifunza mengi kutokana na ziara hiyo.
“Yaani sijui hata niseme nini, maana leo ni kama siamini kumuona Ne-Yo ‘live’, nimepiga naye picha na kumuona akitumbuiza moja kwa moja jukwaani”, alisema Barbara Mawalla, miongoni mwa vijana watano waliokwenda kushuhudia onyesho hilo.
Kwa upande wake, Patricia Kajange alisema, “Nina furaha ambayo hata siwezi kuilezea hapa nilipo, nimefurahi sana kumuona Ne-Yo pamoja na wasanii wengine hawa kama Ali Kiba na Maurice Kirya, nimefurahi sana kwa kweli”.
Hilda pia hakuwa nyuma kuzungumzia furaha yake mara baada ya kupata fursa hiyo, “Yaani nilikuwa nimechoka kutokana na safari lakini baada ya kushudia hili onyesho na kumuona kwa mara ya kwanza Ne-Yo kwa macho yangu mwenyewe, na uchovu wote ukaisha, ni kumbukumbu kubwa sana kwangu”.
Anderson kwa upande wake alisema, “aisee furaha niliyonayo siwezi hata kuielezea kwa sababu ni kama ndoto zimetimia sasa, kumuona Ne-Yo live? sio jambo la mchezo, nawashukuru sana waliofanikisha suala hili”
Annalisa alisema, “nimefurahishwa sana na jinsi wasanii hawa walivyoimba kwa sauti yenye mpangilio na manjonjo ya aina yake, wakiongozwa na Ne-yo, hili ni jambo la kipekee sana kwangu, ni historia nyingine hii katika maisha yangu”.
Baada ya kumalizika kwa onyesho hilo pia vijana hao walipata nafasi ya kukutana na Ali Kiba na kuzungumza naye machache pamoja na kupiga picha ambapo, Ali Kiba aliwaambia amefarijika sana kuwaona vijana kutoka Tanzania maana walimfanya ajisikie yupo nyumbani.
“Nimefurahi sana kuwaona na nimefurahi pia kwa sapoti yenu, ninyi kama Watanzania wenzangu, ningependa kusema kuwa ni muhimu kujituma katika kile mnachokiamini ili mtimize malengo yenu kwa sababu juhudi ndio kila kitu, ndio maana tunasema lazima uwe na sababu bilioni za kuamini”.
Coke Studio Afrika ni onyesho linalofanyika kila kwaka likiwa na lengo la kuwakutanisha kwa pamoja wasanii mbalimbali wa Afrika na kuimba nyimbo ambazo zina vionjo tofauti hivyo kuongeza msisimuko. Lakini vilevile kutoa fursa kwa wasanii wachanga kushirikiana na wakubwa ili kuwapa changamoto ya kuongeza ujuzi katika kazi zao na kuzidi kukuza vipaji vyao.
Mwaka huu, onyesho hilo limeenda bega kwa bega na kampeni ya “Sababu Bilioni za Kuamini” ambayo inalenga kuwahimiza vijana wote kujiamini juu ya ndoto walizonazo na kupambana ili kutimiza ndoto hizo.
Katika msimu huu wa tatu wa Coke Studio Afrika, ni wasanii kutoka mataifa matano tu tu ndio wamechaguliwa kutumbuiza. Mataifa hayo ni Nigeria, Msumbiji, Kenya, Uganda na Tanzania