Member wa kundi la Navy Kenzo na mtayarishaji wa muziki, Nahreel amesimulia maisha na mpenzi wake Aika wanayeunda naye kundi hilo.
Kabla ya kuanzisha kundi la Navy Kenzo, wawili hao walikuwa wakiunda kundi la Pah One na wasanii wengine wawili.
“Mimi na Aika tumekutana tukiwa India masomoni, wote tulikuwa tunasomeshwa na wazazi wetu, tumepitia mambo mengi sana tukamaliza shule na tukaja Tanzania,” Nahreel alikiambia kipindi cha Mkasi cha EATV.
“Mimi nikawa nimeajiriwa na Aika akawa ameajiriwa lakini baadaye tukaona muziki wetu unapotea, kwa sababu tumeingia kwenye kazi nyingine. Kwahiyo tukaamua kuja Dar ili kufanya mambo ya muziki,” aliongeza.
“Kwahiyo tulianza chini sana, tulianza with nothing, nilikuwa na godoro dogo ambalo nilianza na Aika. Tulikuwa tunalala kwenye hilo godoro mimi na Aika. Tukaanza hivyo huku tunafanya muziki. Mimi nafanya production zangu na Aika anafanya shughuli zake za mitindo ndio hivyo tumetokea kwenye vitu vingi tukajenga mpaka hapa tulipofika.”
“Tumepambana sana mpaka kufikia hapa.”