Mshindi wa Airtel Trace Music Star, Mayunga Nalimi amekamilisha Collabo yake na Boss wa konvict Music, Akon huko Hollywood Marekani.
“Nilikua nina siku moja tu yakushika kila kitu kwenye wimbo niliopewa” Mayunga ameiambia TeamTz “Kwahiyo ilinibidi nijitume ili niufahamu vizuri wimbo ili nifanye kitu kizuri hata bwana Akon afurahi na namshukuru Mungu alifurahi sana”
Mayunga amesema kuwa mrembo aliyetumika kwenye video hiyo ni model mkubwa marekani ambaye pia amewahi kutumika kwenye video ya Chris Brown “Huyo video queen ni mkubwa sana kwani amewahi kufanya video ya Chris Brown kama Main character” Amesema Mayunga
Hizi ni baadhi ya picha za Behind The Scene ya Video hiyo