Mzee Abdul Ngarawa Mjumbe wa Kamati ya Maudhui kutoka TCRA akitoa neno la Busara wakati wa warsha hiyo ambapo alisisitiza kuzingatia uzalendo umuhimu wa kutazama utu na staha ya mtu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba (Kushoto) akiongoza majadiliano kwa ujumla ambapo wadau walichangia mawazo na kuuliza maswali mbalimbali
Bwana Daniel Mbega Mmiliki wa Blogu ya Maendeleo Vijijini akichangia mawazo yake wakati wa warsha hiyo
Bw. William Malecela Maarufu kwa jina la Le Mutuz mmiliki Blogu ya Wananchi na Le Mutuz Tv Onine akichangia mambo mbalimbali na kutoa maoni yake wakati wa Warsha hiyo
Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania(TBN) Bw. Joachim Mushi (kulia) akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya waendesha wote wa mitandao kwa TCRA kuendesha warsha hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi James Kilaba pamoja na wadau wengine wakizindua Rasmi Kampeni ya kusisitiza matumizi bora ya Mitandao ya Kijamii awamu ya Pili ambapo Kauli mbiu inasema “Usinitumie Sitaki na Simtumii Mwengine Nitakuripoti”
Baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA Bi. ValerieNdeneingo-Sia Msoka akitoa neno la kufunga wakati wa Warsha hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha hiyo
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania
Paschal Dotto-MAELEZO.
kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini(TCRA) imetia nia kuboresha mawasiliano
kwa umma hasa katika matumizi ya mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watanzania
kupata elimu bora ya maendeleo na kujenga uchumi uliobora.
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka hiyo Dkt. Jonas
Kilimbe alipokua akihutubia hadhara ya
wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (blogu na Online TV) katika uzinduzi wa
kampeni ya awamu ya pili ya “kusisitiza matumizi bora ya mitandao ya kijamii” iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere.
Kilimbe alisema kuwa kwa sasa teknolojia ya mtandao inakua kwa kasi kwa hiyo huduma
za habari zinapatikana kila sehemu kwa njia ya mtandao na kufanya matumizi ya
mitandao kuwa makubwa.
kwa umma imepiga hatua kubwa sana duniani kwa sasa, kwa kiasi kikubwa mtandao
unachangia kuwepo kwa habari nyingi. Tanzania inajumla ya televisheni za mitadaoni
zipatazo 50 pamoja na blogu 150 ambazo zote zinatoa taarifa kwa wananchi, hii
inaashiria kuwa mawasiliano kwa umma yamehamia zaidi kwenye mtandao”, alisema
Dkt.Kilimbe.
kuwa sekta hii inapaswa kuangaliwa zaidi kwani ni sekta muhimu kwa ujenzi wa
Taifa na kuwaasa vijana kutumia vizuri teknolojia hiyo kwa kujielimisha
kuhusiana na masuala ya maendeleo kuliko kutumia vibaya mitandao hiyo.
kubwa kwa sababu sekta hii ya mawasiliano imeshikiria kila kitu na tasnia ya
habari ina nguvu kubwa sana kwa kuleta elimu ya maendeleo kwa wananchi kwa hiyo
waandishi mitandaoni tumieni weledi
mkubwa kwa habari za maendeleo.”, alisisitiza Dkt. Kilimbe.
kuwa katika matumizi ya teknolojia hii mpya yanapaswa kuzingatiwa kwa ajili ya ujenzi wa taifa hasa kwa wale
wanaotumia vizuri mitandao ya kijamii inawapa elimu kubwa ya maendeleo.
amekishukuru chama cha wamiliki wa blogu na televisheni mtandaoni(TBN) kwa
kuleta umoja na kuzingatia maadili na weledi wa umilikajia wa vyombo hivyo kwa
kuwahabarisha wananchi.
mwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadeus Lingo alisisitiza usalama wa matumizi ya
mtandao akisema kuwa idadi ya watumiaji wa mitandao imeongezeka duniani kuanzia
Julai 1, 2017 na kufikia bilioni 3.8 huku kati ya hao bilioni 3.4 ambayo ni
sawa na asilimia 92 ni watumiajia wa mitandao ya kijamii hali iliyosababisha
kuongezeka kwa vyombo vya habari kuhamia mtandaoni, kwa hiyo weledi unahitajika
katika kuhabarisha umma kwa njia hii.