Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza na kusalimiana na Katibu wa NEC itikadi,uenezi na mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Paul Makonda wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia samaki kwaajili ya wavuvi wa kanda ya ziwa.
Hafla hiyo imefanyika leo Januari 30, 2024 jijini Mwanza ambapo vitendea kazi hivyo vimegaiwa kwa wavuvi kwa mkopo usiokuwa na riba ili kustawisha maisha ya wavuvi na kukuza biashara ya samaki.
#KonceptTvUpdates