Mfanyabiashara, Rostam Aziz ameeleza sababu za aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa (Hayati) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambapo alichukua fomu ya kugombea nafasi ya Urais 2015.
Moja ya Sababu zilizopelekea Hayati Lowassa kuchukua uamuzi huo ni kuona hakutendewa haki na kutuma ujumbe hali inatakiwa ibadilike.
“Lowassa alitoka CCM kwenda kugombea nafasi hiyo (urais) kupitia upinzani kwa sababu kuu moja, alikwenda upinzani kwa sababu hakutendewa haki na alitaka kutuma meseji kwamba lazima hali ibadilike,” ameesema Rostam.
#KonceptTvUpdates