Bei ya mafuta kwa mwezi Machi imepanda ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam petroli itauzwa kwa shilingi 3,163 kutoka 3,051 mwezi Februari, dizeli 3,126 kutoka 3,029 na mafuta ya taa yatauzwa shilingi 2,840 kwa lita kuanzia leo Machi 6, 2024.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeeleza kuwa, mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi huu yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 4.5 kwa mafuta ya petroli na asilimia 1.99 kwa mafuta ya dizeli na kupanda kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa 15.38 kwa petroli na asilimia 40.41 kwa dizeli na kwa Bandari ya Mtwara kwa wastani wa asilimia 7.61 kwa petroli na dizeli.
Pia, EWURA imeeleza kuwa, mabadiliko ya bei za mafuta yamechangiwa pia na ongezeko la matumizi ya EURO katika kulipia mafuta yaliyoagizwa.
Cc; Eatv
#KonceptTvUpdates