Jeshi la Polisi MkoaniMorogoro limemfikisha Mahakamani Mohamed Salanga Mkazi wa Kijiji cha Kimamba A Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kwa mashtaka manne likiwemo la mauaji ya Bitrice Ngongolwa.
Mohamed Salanga anadaiwa kumuua mkewe Beatrice Ngongolwa na kumfukia ndani ya chumba walichokuwa wanaishi.
Hata hivyo mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwenye shauri hilo kwasababu Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Mbali ya shauri la mauaji Salanga anakabiliwa na shitaka la kumfanyia ukatili
mtoto wa kike wa marehemu mwenye umri wa miaka 12 kwa nyakati tofauti kuanzia Aprili 2023 hadi Machi
2024.
#KonceptTvUpdates