Kufuatia vifo viwili vya Mwalimu na Mwanafunzi vilivyotokea hivi karibuni mkoani Mbeya, Jeshi la Polisi la Mkoa huo linamtafuta mtu aliyehusika katika tukio la mauaji ya aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi Mbugani Heriety Lupembe (37) na Mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Isenyela Ivon Tatizo (15) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji cha Kiwanja Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
Taarifa ya SACP Benjamin Kuzaga inaeleza kuwa tukio hilo limetokea Machi 31, 2024 majira ya saa 2:30 usiku wakati marehemu akiwa nyumbani kwake sebuleni na watoto wawili Ivon Tatizo na Haris Barnaba Mtweve (06) Mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Shule ya Mchepuo wa kiingeleza ya Ken Gold aliyejeruhiwa kwa kupigwa na kitu butu kichwani.
#KonceptTvUpdates