Klabu ya Simba SC imemtambulisha Mshambuliaji Steven Mukwala raia wa Uganda baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu kutoka Asante Kotoko ya Ghana.
Mukwala mwenye umri wa miaka 24 ni mshambuliaji kinara mwenye uwezo wa kufunga hivyo Simba SC inategemea atakuwa msaada mkubwa kwa timu.
Mukwala amefunga mabao 14 na kuisaidia kupatikana kwa mengine mawili katika michezo 28 katika ligi kuu ya Ghana
Mukwala ana urefu wa futi 5.9 na ana uwezo wa kufunga magoli ya aina yeyote lakini pia ni mzuri kwenye mipira ya juu na mipira ya krosi.
Moja ya eneo ambalo lilikuwa na mapungufu msimu uliopita ni katika safu ya ushambuliaji hivyo ujio wa Mukwala utaongeza uimara wa timu akisaidiana na Fredy Michael Koublan aliyesajiliwa kupitia dilisha dogo.
Mukwala amewahi kuzitumikia timu za Vipers FC, Maroons FC zote za Uganda kabla ya kutimkia Asante Kotoko ya Ghana.
hashtag KonceptTvUpdates