Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff leo tarehe 02/07/2024 ameshiriki katika ukaguzi wa mradi wa Ujenzi wa barabara ya Iringa – Kilolo akiambatana na TANROADS na ujumbe wa Benki ya Dunia.
Mradi huo ni sehemu ya Mradi wa uboreshaji wa barabara vijijini na ufunguaji wa fursa za kiuchumi na kijamii unaotekelezwa na TARURA na TANROADS.
Ujumbe huo wa Benki ya Dunia unatembelea Miradi ya RISE kuona kama utekelezaji wake unaendelea kulingana na Mpango wa utekelezaji uliokubalika na kuona changamoto katika utekelezaji kama zipo.
Mradi wa ujenzi wa barabara ya Iringa (Ipogolo)-Kilolo (33.61) ni wa kiwango cha lami unatekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) na Mkandarasi China Henan Engineering Company.