Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Ndg. Togolani Edriss Mavura amethibitisha kupokea ugeni wa Wasanii wa Filamu Tanzania nchini humo na kufanya mazungumzo ya namna ya kuendeleza ushirikiano na Korea kusini ili kupata ujuzi na uzoefu zaidi katika kukuza Tasnia ya Filamu nchini Tanzania.
“Nimefanya mazungumzo na wasanii wa filamu wa Tanzania waliofika Ubalozini leo asubuhi. Wasanii wetu wako nchini Korea Kusini ikiwa ni maelekezo na matokeo ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. @SuluhuSamia nchini Korea Kusini ambapo pamoja na mambo mengine, alianzisha mazungumzo ya kupanua njanya za ushirikiano katika sekta ya filamu kati ya Tanzania na Korea Kusini.
Tanzania na Korea Kusini zinashirikiana katika sekta ya filamu kupitia MoU kati ya Jiji la Busan (Busan Global Citizenship Foundation) na Bodi ya Filamu Tanzania; na Mpango wa Mafunzo wa Miaka 3 wa Sekta ya Filamu (2024-2027) kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA).