Menejimenti ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA), ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Patrick Kibasa imetembelea maeneo matatu yanapojengwa matenki ya mradi huo yenye uwezo wa kuhifadhi Maji jumla ya lita millioni 9.
Mhandisi Kibasa alimwambia Mkandarasi ahakikishe anakamilisha ujenzi wa matenki hayo kufikia mwezi Desemba 2024, kama alivyoahidi kwa kuwa ameshalipwa zaidi ya shilingi bilioni 21 kama fedha ya kuanza kutekeleza mradi hivyo hakuna kisingizio chochote cha kuchelewesha mradi huo.
Vilevile, alimwambia Mkandarasi awasilishe kwa wakati usanifu wa kidaka maji pamoja na mtambo wa kuchuja na kutibu maji ili Wizara na Mhandisi mwelekezi waweze kuidhinisha na ujenzi uweze kuendelea bila kusimama.
Lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha Miji yote inafikiwa na huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2025.