Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Stanslaus Nyongo amesema Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu (Sabasaba) ni fursa muhimu ya kutangaza na kuwakaribisha wawekezaji ili kuona fursa mbalimbali za uwekezaji nchini.
Ameongeza kuwa Maonesho hayo yamekuwa na mvuto mkubwa kwa kuwa Wizara na taasisi zilizoshiriki zimeonesha fursa zilizopo katika uwekezaji.
“Tanzania tunaona hii ni fursa nzuri ya kujitangaza kama nchi na kukaribisha wawekezaji mbalimbali kuona fursa za uwekezaji katika nchi yetu” amesema Mhe.Nyongo
Aidha, amepongeza namna ambavyo wafanyabishara wamekuwa wabunifu na makampuni ya nje yaliyokuja kuonesha shughuli za uwekezaji wanazoweza kufanya nchini.
#KonceptTvUpdates