Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) ameshiriki Mkutano wa Maandalizi wa Kongamano la Tisa la Diaspora baranı Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao.
Mkutano huo wa Umoja wa Afrika wa maandalizi kwa ajili ya Kongamano la Tisa kuhusu Diaspora wa Afrika na wenye Asili ya Afrika litakalofanyika nchini Togo baadaye mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mbarouk, aliuthibitishia mkutano huo kuwa Tanzania inaunga mkono Kongamano hilo na malengo yake lililopangwa kufanyika nchini Togo.
Amesema Umoja wa Afrika na Mashirika ya Kikanda yamechukua hatua kadhaa kukuza na kuimarisha matumizi ya lugha za Kiafrika na tamaduni zake ikiwa ni pamoja na kutumia lugha ya Kiswahili katika ngazi za kitaifa, kikanda na kimataifa.
Amesema jitihada hizo zililiwezesha Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuitangaza tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.
“Haya ni mafanikio makubwa kwa Afrika, Kiswahili kimekuwa moja ya lugha zinazotumika sana kutoka familia ya lugha za Kiafrika duniani ikiwa na zaidi ya wazumgumzaji milioni 230, na kuwa miongoni mwa lugha 10 zinazozungumzwa zaidi duniani, alisema Balozi Mbarouk.
Cc:W/Mambo ya Nje