Kijana Kasala Lugole mwenye umri wa miaka 20, mkulima na mkazi na Nduguti, Wilaya ya Mkalama mkoani Singida amehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo Disemba 12, 2017 majira ya usiku katika kijiji cha Kinyangiri Wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Novemba 23, 2022.
Aidha, hukumu hiyo imetolewa Julai 08, 2024 na Mahakama ya Mkoa wa Singida mbele ya Mhe. Jaji E. Kakolaki .J. baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa na upande wa Jamhuri.
Cc; Police Tanzania (Instagram)
#KonceptTvUpdates