NA MWANDISHI WETU
Kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan ya Kobe Motor,imetoa zawadi mbali mbali kwa wateja wake ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na wateja pamoja na kusherehekea mafanikio yake.
Ikiwa ni moja kati ya makampuni makubwa ya Kijapan yanayoongoza kwa kuuza magari kwa ajili ya matumizi binafsi na ya kibiashara sehemu mbali mbali duniani,Kobe Motor tayari imeshauza magari zaidi ya 150,000 hapa Tanzania.
Akiongea wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wateja wake, mkuu wa kitengo cha masoko Ken Aoki alisema mafanikio ambayo kampuni hiyo imeyapata ni kutokana na wateja wake waaminifu.
“Leo tunajivunia kampuni yetu kutokana na ukubwa wake pamoja na uwezo wa kuwafikia maelfu ya wateja hapa Tanzania na sehemu nyingine duniani. Mafanikio haya tunayojivunia yamepatina kutokana na wateja hawa ambao leo tumejumuika pamoja kusherehekea mafanikio,” alisema mkuu huyo wa masoko.
Katika hafla hiyo ya chakula cha jioni, iliyoambatana na burudani mbali mbali,ilichezeshwa droo ambapo wateja wa Kobe Motor walijishindia zawadi mbali mbali kama simu za mkononi,tablet, komputa mpakato (lap top).
Mmoja wa wateja wa kampuni hiyo aliyejitambulisha kama Dallas Mulamba alisema amekuwa akikafanya biashara na Kobe Motor kwa miaka zaidi ya mitano na kwamba huduma bora za kampuni hiyo zimemsaidia kukuza biashara yake.
“Biashara ya kuagiza magari ina changamoto zake kwa kuwa unaagiza kwa kuona picha tu. Wakati mwingine picha hudanganya na makampuni yasiyo na uaminifu hutuma picha nzuri lkn gari likifika hali inakuwa tofauti. Lkn nikiagiza na Kobe Motor huwa sina shaka maana unachokiona kwenye picha ndicho utakachokipokea,” alieleza
Katika hatua nyingine hiyo ilitangaza kuwa imeanzisha huduma ya kuuza magari kwa mfumo wa mteja kutoa asilimia 35 ya thamani ya gari na kiasi kilichobaki anaweza kulipa kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi miwili. Lengo la mpango huo ni kuwawezesha wateja wenye mahitaji ya magari lakini hawana fedha za kulipa mara moja kuweza kupata magari ya ndoto zao.
Mkuu wa Masoko wa Kobe Motor, kampuni inayouza magari
yaliyotumika kutoka Japan Ken Aoki (wa pili kushoto) akimkabidhi mmoja wa
wateja wa kampuni hiyo Ucaya Awanga zawadi mara baada ya kuibuka mshindi katika
droo iliyofanyika jijini Dar es Salaa wakati wa chakula cha jioni
kilichoandaliwa na kampuni hiyo kwa aji ya wateja wake. Kushoto ni Muhammed
Fahmi, ambaye ni afisa mauzo mwandamizi wa Kobe Motor.
Maneja wa kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan
ya Kobe Motor Ananda Shanka akimkabidhi
mmoja wa wateja wa kampuni hiyo Vimal Patel zawadi mara baada ya kuibuka
mshindi katika droo iliyofanyika jijini Dar es Salaa wakati wa chakula cha
jioni kilichoandaliwa na kampuni hiyo kwa aji ya wateja wake. Anayeshuhudia
kushoto ni Muhammed Fahmi, ambaye ni afisa mauzo mwandamizi wa Kobe Motor.
Muhammed Fahmi (kushoto) Afisa mwandamizi mauzo kutoka
kampuni ya Kobe motor Japan inayouza magari yaliyotumika kutoka Japan
akimkabidhi zawadi Mohamedraya Hassam ambaye ni mteja wa kampuni hiyo mara
baada ya kuibuka mshindi katika droo iliyofanyika jijini Dar es Salaa wakati wa
chakula cha jioni kilichoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake.
Kushoto ni Mkuu wa Masoko wa Kobe Motor Ken Aoki.
Bendi ya Violist ikitumbuiza wakati wa hafla ya chakula cha
jioni iliyoandaliwa na kampuni ya kuuza magari yaliyotumika kutoka Japan ya
Kobe Motor kwa ajili wateja wake na kufanyika katika hotel ya Hyatt Regency ya
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Masoko wa Kobe Motor, kampuni inayouza magari
yaliyotumika kutoka Japan Ken Aoki ( kulia) akiwa na Muhammed Fahmi (kushoto) ambaye
ni afisa mwandamizi mauzo wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya wateja muda mfupi baada ya hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na
kampuni hiyo kwa ajili ya wateja wake.