Ripoti ya uchunguzi iliyofanywa na wataalamu wa miamba kutoka Taasisi ya Geolojia na utafiti wa madini Tanzania (GST), kwa kushirikiana na TANROADS, na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufuatia mpasuko wa ardhi na kuporomoka kwa tuta la barabara uliojitokeza katika eneo la Busunzu lenye urefu wa mita 200, Mkoani Kigoma haijatokana na makosa ya Mkandarasi kwenye ujenzi bali umesababishwa na sababu za kijiolojia.
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kuwa uchunguzi umebaini mpasuko wa ardhi na kuporomoka kwa tuta la barabara uliojitokeza katika eneo la Busunzu lenye urefu wa mita 200 haijatokana na makosa ya Mkandarasi kwenye ujenzi bali umesababishwa na sababu za kijiolojia
Amebainisha kuwa kipande cha barabara hiyo kipo katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Manyovu – Kasulu – Kibondo – Kabingo Awamu ya tatu ya barabara ya Mvugwe hadi Makutano ya Nduta (km 59.35) ambayo ilikwishakamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Bashungwa ametoa taarifa hiyo Mkoani Kigoma leo Julai 10, 2024 mara baada ya kukagua eneo hilo na kupokea taarifa ya uchunguzi iliyofanywa na Wataalamu wa miamba kutoka Taasisi ya Geolojia na utafiti wa madini Tanzania (GST), Kitengo maalum cha Utafiti cha TANROADS, na School of Mines and Geosciences (SoMG) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
“Nimepokea taarifa za kitaalamu na nimejionea zaidi ya mita 200 namna ambavyo majanga ya asili yaliyoathirika eneo hili, Serikali iliunda jopo la kufanya utafiti wa kina kuanzia mwezi Februari na tulichokigundua hapa sio makosa ya Mhandisi, sio upigaji kama watu wengine walivyodhani”, amesema Bashungwa
#KonceptTvUpdates