Tangu Aziz Ki alipojiunga na klabu ya Yanga msimu wa 2022/2023, mashabiki wa soka hasa hasa wa Yanga wamekuwa na kitu cha ziada cha kufurahia kila mechi. Kijana huyu mwenye kipaji cha kipekee amekuwa kielelezo cha ustadi, umahiri, na uhodari kwenye timu ya Yanga SC. Kila mara anapokanyaga uwanja, ni kama nyota inayong’ara usiku wa giza kwa washabiki wa Yanga.
Aziz Ki alijiunga na Yanga SC akitokea ASEC Mimosas, klabu maarufu ya soka kutoka Ivory Coast akiwa na matumaini makubwa, na mara moja alianza kuonyesha uwezo wake. Kutoka kwa pasi za kiufundi, mbinu za kuvutia, hadi mabao ya kuvutia, Aziz Ki amekuwa mchezaji ambaye kila mshabiki wa Yanga anajivunia kumuita wao. Kila goli na kila dribbles zake zimekuwa zikiwapa mashabiki furaha na matumaini ya ushindi.
Wakati mwingine, kile kinachomfanya Aziz Ki kuwa maalum zaidi ni roho yake ya kiushindani na bidii yake uwanjani. Hachoki, hakatishi tamaa, na kila wakati anatafuta namna ya kuiboresha timu yake.
Hapa chini ni Highlights za Aziz Ki Akiwa na Yanga kwenye ubora wake.
Kutazama video hii ya “Best Moments za Aziz Ki akiwa na Yanga” ni kurudisha nyuma wakati wa furaha, ushindi, na ustadi wa kipekee. Karibu utazame na ufurahie kila dakika ya kipaji hiki cha kipekee!