#USAJILI: Young Africans Sc imefanikiwa kunasa saini ya kiungo Duke Abuya (30) raia wa Kenya kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na Singida Black Stars FC kumalizika.
Abuya anakuwa mchezaji wa sita kutua katika viunga vya Jangwani baada ya waliotambulishwa awali ambao ni Prince Dube, Khomeiny Aboubakar, Clatous Chama, Chadrack Boka na Aziz Andambwile.
#KonceptTvUpdates